Canalblog
Editer l'article Suivre ce blog Administration + Créer mon blog
Publicité
zone verte
zone verte
Archives
Derniers commentaires
3 août 2008

Kurudi Ufaransa...

Nimeshafika Ufaransa, "Peponi" kwa maoni ya watu wachache...

Kwa mimi siyo peponi : mvua, shida za kisiasa, watu wanaokimbia daima, na pia wanahabari wanaoendelea kuandika kuhusu rais wetu kila siku... Kusema kweli, nimeshachoka.

Nyinyi wote ninawamisi sana.

Nataka kuwashukuru kwa urafiki wenu, hata upendo wenu, ukaribisha wenu, msaada tena, kila tabasamu, na kutumia wakati mzuri na sisi. Kweli kila mwimbo unabaki kichwani kwangu, kila neno, kila tendo. Bila nyinyi, safari hiyo ingalikuwa tofauti kabisa, yaani siyo nzuri kama hivi.

Mungu awabariki sana, nyinyi na familia zenu, kwa milele.

Tutaonana insha'allah, Mungu akipenda, na nyinyi mkipenda.

Tutafanya kazi kwa bidii kushinda (siyo kupwewa!) mradi wetu kufungua kituo cha utamaduni mjini Bagamoyo. Huko ni Peponi kwa mimi :)

Ahsante kuamini kwamba kuna mahusiano kati ya watu mbalimbali (kutoka Afrika na Ulaya) nje ya biashara na utalii tupu. Nimefurahi sana moyoni mwangu kuwakuta na nyinyi.

Nisamehe kwa makosa ya kiswahili...

Mwanafunzi Amani - Laurène - Naseriani - Mwajuma - Fatuma ... labda nimesahau jina... :)

Kila la heri

Publicité
Commentaires
A
Karibu mpenzi wangu!!<br /> Bientôt tu seras là-bas avec moi, tutaenjoy sana!<br /> <br /> Nakupenda kima yangu :)
D
Bravo pour la beaute des photos et la qualite de tes textes, tu nous fais voyager par la pensee.
Publicité
Publicité