Canalblog
Editer l'article Suivre ce blog Administration + Créer mon blog
Publicité
zone verte
zone verte
Archives
Derniers commentaires
5 avril 2008

« Anthropolojia si spoti ya hatari », Nigel Barley

« Maarifa ya makabila huwasaidia wanajeshi kufanya kazi ya ufanisi na kutotumia silaha ». Hiyo ni pendekezo la kazi, ili kuwashawishi wanaanthropologojia wanaotafuta kazi kufuata jeshi la kimarekani. Hivyo ndivyo ni ratiba ya HTS, Human Terrain System, ilipangwa na serikali ya kimarekani.

Human Terrain System ni ratiba ya serikali ya kimarekani, inayowashirikisha wanaanthropologojia na wajeshi, nchini Irak na Afghanistan. Ingesemekana « embedded anthropologists », kama ilivyosemekana kuhusu wanahabari waliokuwa wanafuata wajeshi, wakati wa vita ya pili nchini Irak. Ratiba hiyo inawatilia wasiwasi wanaanthropologojia wengi, kwani inafanana na ratiba nyingine za zamani.

Siyo ratiba mpya

Kwa mfano, wanaanthropologojia walifanya kazi pamoja na viongozi kipindi cha ukoloni, mwishoni mwa karne kumi na tisa. Walifanya utafiti kuhusu « makabila » mbalimbali, ili wawasaidie viongozi kuwatawalisha wenyeji wa asili, kwenye koloni za Uingereza na za Ufaransa. Wakijua mila na tabia za watu, wakoloni waliweza kuongoza waafrika rahisi sana.

Vile vile ni hali ya vita mbili za kimataifa. Wanaanthropologojia kama Margaret Mead, Gregory Bateson na Ruth Benedict walikupa maarifa yao kundi la nchi zilizokuwa zinashirikiana. Miongoni mwa utafiti wengine, walifanya utafiti sehemu ya Asia.

Mwaka 1965, ratiba ya Camelot ilipangwa kutafuta sababu za ukali nchini Chili. Ratiba ya Civil Operations and Revolutionary Development Support (Cords) ilikuwa inawasaidia wamarekani kuwajua wavietnami ambao wangeweza kuunga mkono wakoministi.
Hali hizo zilibishiwa na mwanzisha wa sayansi ya jamii, Franz Boas, kwenye gazeti la The Nation, mwaka 1919. Alikosoa mienendo ya wanaanthropologojia kadhaa kipindi cha vita ya kimataifa ya kwanza. Alifukuzwa kazi na skirika la wanaanthropologojia wa kimarekani (AAA). Siku hizi, shirika hilo ndilo linashtumu ratiba ya HTS... AAA imebadilika mawazo yake mpaka kutia mwandika wa kideontolojia kwa wanaanthropologojia wote mwaka wa 1970.

Mwandiko wa kideontolojia wa wanaanthropologojia

Kama madaktari na wanahabari, wanaanthropologojia wanaheshimu mwandiko wa kideontolojia. Hawaruhusiwa kutumia utafiti wao dhidi ya watu na wanalazimishwa kuwaarifu watu kila mara wanapofanya utafiti kuhusu wao. Basi ratiba ya HTS ilipangwa ili wanaanthropologojia wafanye kazi pamoja na wajeshi, yaani ili utafiti wao wawasaidia watu kuwa na imani na wajeshi. Vita ni rahisi zaidi watu wanapowaamini maadui.

Wanaanthropologojia waliofanya kazi pamoja na jeshi hutangaza kwamba kwa kweli walibadilisha mwenendo wa wajeshi kwa mujibu wa mila mbalimbali. Wengine huwajibu wananyofu kuamini serikali. Wote wanakubali kufungua kituo kikubwa cha utamaduni, lakini kikitumiwa na jeshi itakuwa shida. Mfumo wa Network of Concerned Anthropologists imebuniwa kupinga ratiba ya HTS. Kama alivyosema mwandishi Nigel Barley: « Antropolojia si spoti ya hatari », inategema jinsi inavyotumiwa...

Publicité
Commentaires
Publicité
Publicité