Canalblog
Editer l'article Suivre ce blog Administration + Créer mon blog
Publicité
zone verte
zone verte
Archives
Derniers commentaires
2 août 2008

Majengo yanapoota mpaka angani

Inaonekana kwamba watu hupenda siku hizi majengo marefu sana. Suali la jinsi tunavyojenga nyumba limezuka tangu zamani. Lakini siku hizi, limefikia kipeo chake. Na inasababisha matatizo ya kijamii na ya hifadhi ya mazingira. Mifano michache duniani popote.

Bahrein ni kisiwa kidogo karibu na Saudi Arabia. Huko wajenzi huvumbua  majengo yanayotoka ndotoni mwao. Ukipanda ndege kwenda Manama, mji mkuu wa Bahrein, utaona kwanza majengo marefu ya ajabu. Moja lenye ncha kama mdomo wa ndege, moja lenye balbu kama mti wa Krismasi, jingine lenye rangi inayobadilikabadilika. Kujenga majengo hayo, Wahindi wengi waliingizwa nchini, kama maelfu ya siafu. Lengo pekee lilikuwa kujenga haraka haraka na kujenga nyumba nyingi. Ila shida ni kwamba majengo hayo siyo imara na hayadumu miaka mingi. Kama vile fast-food yaani chakula kinachopikwa haraka, kuna fast-nyumba, nyumba zinazojengwa haraka : unapomaliza kuishi pale, nyumba unaitupa kama soksi mbovu. Waindia watajenga nyingine.

Utandawazi

Mjini Misri, watu huhitaji Wahindi. Hujenga nyumba zao wenyewe. Matokeo ni kuwa majengo marefu huota bila ruhusa ya kujenga wala kuheshimu kanuni za usalama. Hivi karibuni, jengo moja lilibomoka. Lakini hali hiyo ni matokeo ya hali nyingine : serikali haikuwepo. Misri kuna watu chungu nzima na hakuna nyumba za kutosha. Ni lazima kujenga wenyewe miundombinu.

Kuna sababu nyingine : pawe Misri, Bahrein, au Kinshasa, popote watu hutaka kuiga nchi za Magharibi. Kwa hivyo majengo marefu yanatanda hata katika miji ambayo ni maskini sana, lakini wanapoiga mtindo huo wa kujenga nyumba, wanaiga vile vile shida zote zinazoambatana na ujenzi wa aina hiyo yakiwemo matatizo ya kijamii na shida za kutohifadhi mazingira.

Majenga marefu, matatizo makubwa

Tukiendelea na mfano wa Misri, kuna kitongoji kimoja kinachofanana na vitongoji vinavyozunguka Paris. Majengo marefu kama Minara ni kama vile Ufaransa. Shida pia. Kuishi katika minara hakusaidii kukutana na majirani wake. Mandhari si nzuri, kwa hivyo hakuna mtu mmoja anayetembeatembea nchini ya majengo. Kwa jumla, hakuna tena miti, nyasi, hata magugu. Mara kwa mara takataka tu hulundikana, na mivutano vile vile.

Sababu ni dhahiri : Ufaransa majengo hayo yalijengwa kwa muda mfupi tu ili kuwapokea wafanyakazi wahamiaji ugeni. Baadaye, wageni wamekuwa wafaransa, familia zao zikawafuata, na wote hukaa katika vitongoji hivyo. Lakini ni pahali pa kulala tu, siyo pa kuishi. Kukata tamaa, ukiongezea kutoona vizuri siku za mbele zitakavyokuwa kwa sababu ya ukosefu wa ajira kwa wageni na hata wenyeji... Kwa Kuiga majengo hayo, nchi huiga wakati ule ule shida hizo. Nchini Luxembourg tu walifahamu siyo hali ya kuiga. Huko miundombinu huwa na urefu wa binadamu. Kwa wale ambao si tajiri, kuna nyumba ndogo katikati ya mazingira yenye majani na miti, yaani ghorofa mbili tu. Kuishi kwenye mazingira ya msingi ya binadamu ni muhimu sana. Kwa hivyo kujenga nyumba lazima kutegemee kuhifadhi mazingira.

Changamoto kipya : mazingira yahifadhiwe

Luxembourg ni mfano wa kuvutia. Wajenzi hujaribu kuhifadhi mazingira. Hupanga kikusanya cha jua paani, na miundombinu zinazoyorejeleza hewa ya nje kufanya hewa joto ndani ya nyumba. Pia Ufaransa kuna nyumba zinazohifadhi mazingira. Mkoa wa Essonne, Kusini Mashariki mwa Paris, kuna chama cha watu wanaopenda sana anga, chama kinachoitwa “Chama cha wale wanaolinda anga ya usiku”. Hueleza kwamba kuwasha taa za mtaani wakati wa usiku huharibu mazingira, huwatisha ndege, huwazuia watu wanaopenda anga ya usiku kuiangalia. Watu wa chama hicho wanapendekeza taa zinazooanishwa mazingira. Kwa mujibu wao, ni pahali pa kuishi pazuri panahifadhi watu na mazingira.

Publicité
Commentaires
Publicité
Publicité