Canalblog
Editer l'article Suivre ce blog Administration + Créer mon blog
Publicité
zone verte
zone verte
Archives
Derniers commentaires
1 août 2008

Lini mapinduzi ya wanaume ?

« Mapinduzi ya wanawake » ni dhana inayounga mkono wanawake duniani. Ni dhana ya kisiasa, ya kifalsafa, ya kijamii inayotetea haki za wanawake, inayotaka kuboresha hali ya wanawake ulimwenguni. « Mapinduzi ya wanawake » yalitokea kwenye nchi nyingi, lakini sasa Ufaransa chama hicho hakifai hata kidogo.

Kwenye jamii ya kijadi nyingi, wanawake hawakuhusiki mambo ya ngazi ya juu (siasa, uchumi...) Lengo lao lilikuwa kuzaa tu na kubadilishanwa na mahari. Hakuwa na haki ya kupiga kura au kutaliki.
Ufaransa, wakati wa mapinduzi (1789), wanasiasa wachache waliipa nchi matini muhimu sana, iliyonakiliwa na nchi nyingine : « Tangazo kwa wote la haki za binadamu na raia ». Kwa kifaransa, maneno ya « binadamu » na « wanaume » ni yale yale. Mzozo huo wa msamiati ulimpa Olympe de Gouges fikra ya kuandika matini nyingine : « Tangazo kwa wote la haki za wanawake na raia wa kike », mwaka 1791. Mtu wa kimapinduzi wa kwanza.

Kumbuka...
Miaka mia miwili baadaye, mtu mwengine alitumia dhana ya « Mapinduzi ya wanawake » : Simone de Beauvoir. Alipambana kwa ajili ya haki za wanawake. Alifananisha ndoa na ubembe, hali wanawake wanapokuwa watumwa wa mume wao. Yule mwamamke alikuwa mtu wa kwanza kutetea haki ya kuharibu mimba, iliyozingatiwa wakati huo kama mauaji. Simone wengine, yule anayoitwa Veil, alichukua pigano hilo kwa haki ya kuharibu mimba na akaatharisha upigaji kura wa sheria iliyoruhusu kutoa mimba. Ilikuwa mwaka wa 1975.

Dhana ya « Mapinduzi ya wanawake » ikatanda dunia, na nchini Ufaransa, wanawake waliruhusiwa kupiga kura mwaka 1944.

2007 : njia ya chama cha « Wala danguro wala watumwa »... mpaka serikalini
« Wala danguro wala watumwa » ni chama muhimu sana, kwani kinaonyesha maendeleo ya hali ya wanawake nchini Ufaransa. « Wala danguro wala watumwa » imezaliwa mwaka 2000, ili kuunga mkono wanawake kwenye vitongoji. Ni chama cha Fadela Amara na wanawake wanaotoka vitongoji vya Paris kwa jumla. Pingano lake linahusu ukali na uporaji wasichana wanaouvumilia.

Mwaka uliopita kazi ya chama cha « Wala danguro wala watumwa » kilipata shukrani : rais mpya Nicolas Sarkozy akampa Fadela Amara madaraka ya katibu wa serikali anayeshughulikia mambo ya siasa ya miji. Nicolas Sarkozy alitangaza rekebisho kwenye mambo ya kisiasa : akawapa wanawake saba madaraka ya juu serikalini. Hata wanampa sasa shida ndogo kila mwezi. Wanawake wa serikali wana fikra za siasa binafsi. Wasipokubaliana na tabia ya rais, humwambia mbele ya wanahabari. Labda hivyo ndivyo ni « Mapinduzi ya wanawake » : fursa ya kuonyesha fikra zake kwa sauti wakati wanaume wa serikali hawawezi... Kwa hivyo kwa maoni yangu sasa « Mapinduzi ya wanawake » hayafai hata kidogo. Pingano lake siku hizi ni haki za wanawake zizidi haki za wanaume. Na leo kwa kweli wanaume ni watumwa wa wanawake.

« Mapinduzi ya wanawake » : uhuru wa kuzaa bila wanaume ?
« Watoto asilimia hamsini wamezaliwa nje ya ndoa : ni vizuri sana ! » Sentensi hiyo ni ya Isabelle Alonzo, kwenye tangazo la televisheni ya kifaransa. Aliandika kitabu kuhusu uhusiano kati ya wanawake na wanaume. Kitabu chake kilitolewa mwezi huu. Vipi anaweza kutangaza kwamba ni vizuri kuzaa usipokuwa na mume ? Anajuaje kwamba sehemu ya Paris, jozi asilimia hamsini huachana ! Hali hiyo si vizuri, hata kwa « uhuru » wa wanawake, hata kwa raha ya watoto... Siku hizi, wanawake wakifanya kazi wanapata hela yao, na kwa mujibu yao, hivyo ndivyo uhuru ulivyo. Hawahitaji tena mume kununua chakula, kuzaa (kwa msaada wa benki la shahawa), kuamua uamuzi.
Lakini uhuru ni pia kupendwa, kuheshimwa na mumewe, tena kuheshimu mumewe. Inaonekana kwamba kwa jina la « Mapinduzi ya wanawake », wanawake hucheza sehemu mbili : ya mke na ya mume. Mume ni kama mtoto tu. Unaweza kuwaona madukani : mke mbele, mume nyuma. Mwanamume anafuata tu. Haamui hata kidogo. Na mara kwa mara, anapofanya mzaha, mke anamkaripia. Lini mapinduzi ya wanaume ?

Publicité
Commentaires
A
tumepoteza watoto wengi kuingia kwenye magenge yasiofaa uvutaji wa bangi na madawa yakulevya,sitaki kuingilia uhuru wa watu wa ulaya naomba mungu yasienee huku kwetu afrika sababu tutapata shida kama wanaume waulaya walivyokua,wamekua wanawake katika nyumba, na sii wanaume katika nyumba, hawana maamuzi ya famili wenye maamuzi na familia zao ni taasisi za haki za wanawake na watoto, wanaume wa ulaya warudishiwe mamlaka za malezi na mamlaka za kuongoza familia lakini wakumbuke haki zawanaowaongoza na upendokwa ujumla na ndipo hapo upendo na amani utakaporudi tena <br /> Haya ndiyo maoni yangu kwa haki zawanaume zilkizo chukuliwa<br /> Afzal Shah
A
wanawake wamekuwa waamuzi wanyumba loloteanalotaka anafanya pakasasa tunashuhudia katika nchi za ulaya hata baadhi ya nchi za afrika wanawakewanaoana wenyewe kwa wenyewe {lesbin),talakazimekua nyingi mahakamani,ndoa muda ,watoto kuzaliwa nje ya ndoa ,utoaji wa mimba,kutupa watoto, yote imekuja baada kupewa haki kupita kiasi wanawake na watoto nakuchukua mila zamagharibi ambazo hazina maadili isipokua ni kuiangamiza dunia kwa kuwanyima haki zamalezi wanaume ambao ni kicwa cha nyumba sasa famili za ulaya zinayumba mtoto akikosa ukimuadhibu unashitakiwa kwa kuvunja haki za mtoto tunaona
Publicité
Publicité